SOMO: ```MALEZI YA KIMKAKATI.```
📗📗📗📗📗📗📗📗📗
🤽🏻♂️Kijana mmoja aliomba kazi ya umeneja katika kampuni moja. Alifaulu mahojiano ya awali, na kupata nafasi ya kukutana na Mkurugenzi kwa mahojiano ya mwisho.
Siku ya Mahojiano Mkurugenzi aliuliza,
```"Je, ulipata ufadhili wowote wa shule?" kijana akajibu "hapana". "Baba yako ndiye aliyekulipia ada ya shule?"
"Baba yangu alifariki nikiwa na mwaka mmoja, mama yangu ndiye alinilipia karo ya shule," alijibu.```
✒ "Mama yako anafanya kazi wapi?" "Mama yangu anafanya kazi ya kufua nguo." Mkurugenzi alimwomba kijana aoneshe mikono yake. Kijana akaonesha jozi ya mikono ambayo ilikuwa laini na kamilifu. "Je, umewahi kumsaidia mama yako kufua nguo kabla?" Mkurugenzi alihoji.
😭 _“Kamwe, mama yangu sikuzote alitaka nijifunze na kusoma vitabu zaidi. Isitoshe, mama yangu anaweza kufua nguo haraka kuliko mimi._
💡 ```Mkurugenzi akasema, “Nina ombi. Ukienda nyumbani leo, nenda ukasafishe mikono ya mama yako, kisha tuonane kesho asubuhi.
Kijana aliona kuwa nafasi yake ya kupata kazi ilikuwa kubwa. Aliporudi nyumbani, alimwomba mama yake amruhusu kusafisha mikono yake. Mama yake alijisikia furaha lakini akiwa na hisia mchanganyiko, alinyoosha mikono ili kijana aisafishe.
Kijana alisafisha mikono ya mama yake polepole. Chozi lilidondoka kila alivyoendelea kuisafisha mikono ya mama yake. Ilikuwa ni mara ya kwanza kuona mikono ya mama yake ilikuwa imekunjamana sana, na kulikuwa na michubuko mingi mikononi mwake. Michubuko mingine ilikuwa inauma na mama yake alihisi maumivu kila ilipoguswa.```
Hii ilikuwa mara ya kwanza kwa kijana huyo kutambua kwamba ni jozi hii ya mikono ndiyo inayofua nguo kila siku ili kumwezesha kulipa karo ya shule. Michubuko katika mikono ya mama ilikuwa ndiyo malipo ya elimu yake na hata maisha aliyonayo.
Baada ya kusafisha mikono ya mama yake, kijana huyo alifua nguo zote zilizokuwa zimebaki. Usiku huo, mama na mwana walizungumza kwa muda mrefu sana. Asubuhi iliyofuata, kijana alienda ofisini kwa mkurugenzi.
Mkurugenzi aliona machozi katika macho ya kijana huyo, akamuuliza: "Je, unaweza kuniambia ni nini umefanya na kujifunza kwa tukio la jana nyumbani kwenu?"
Kijana akajibu, "Nilisafisha mikono ya mama, na pia nikamaliza kufua nguo zote zilizokuwa zimebaki." "Sasa najua na nathamini hili. Bila mama yangu, nisingekuwa hivi nilivyo leo. Kwa kumsaidia mama yangu, sasa ninatambua jinsi ilivyo vigumu na ngumu kufanya kitu peke yako. Na nimekuja kufahamu umuhimu na thamani ya kusaidia familia.
Mkurugenzi alisema, “Hiki ndicho ninachotafuta kwa meneja. Ninataka kuajiri mtu ambaye anaweza kuthamini msaada wa wengine, mtu anayejua mateso ya wengine ili kufanya mambo, na mtu ambaye hawezi kuweka pesa kuwa lengo lake pekee maishani.”
“Umeajiriwa.”
Kijana huyu alifanya kazi kwa bidii sana, na akapokea heshima ya wasaidizi wake. Kila mfanyakazi alifanya kazi kwa bidii na alifanya kazi kama timu. Utendaji wa kampuni uliimarika sana.
Mtoto, ambaye amelelewa kwa kudekezwa akipewa chochote anachotaka kamwe hujiweka kwanza kwa kila jambo na kila wakati. Anakuwa hajui juhudi za mzazi wake.
Anapoanza kazi, anafikiri kwamba kila mtu lazima amsikilize, na anapokuwa meneja, hatajua mateso ya wafanyakazi walio chini yake na daima atakuwa mtu wa kulaumu wengine. Kwa watu wa aina hii, ambao wanaweza kuwa wazuri kielimu, wanaweza kufaulu kwa muda.
Watanung'unika na kujaa chuki na kupigania zaidi. Ikiwa sisi ni wazazi wa aina hii wanaolinda, je, kweli tunaonesha upendo au tunaharibu watoto wetu? Unaweza kumruhusu mtoto wako aishi katika nyumba kubwa, kula chakula kizuri, kujifunza kuogelea, kutazama mpira (sijui timu gani).
Lakini unapokata nyasi, tafadhali waruhusu wapate uzoefu. Baada ya chakula, acha waoshe sahani na bakuli zao pamoja na ndugu na dada zao. Sio kwa sababu huna pesa za kuajiri mjakazi, lakini ni kwa sababu unataka kuwapenda kwa njia sahihi.
Unataka waelewe, hata wazazi wao wawe matajiri kiasi gani, siku moja nywele zao zitakua mvi, sawa na mama wa huyo kijana. Jambo muhimu zaidi ni kwamba mtoto wako anajifunza jinsi ya kuthamini juhudi na uzoefu wa ugumu na kujifunza uwezo wa kufanya kazi na wengine ili kufanya mambo.
AKILI YA MAFANIKIO
📘📘📘📘📘📘📘📘📘
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
share with us