Lebo

Jumamosi, 25 Septemba 2021

SCHOLARSHIPS TENABLE IN THE ARAB REPUBLIC OF EGYPT FOR THE ACADEMIC YEAR 2021/2022

 Call for Application

The general public is hereby informed that the Egyptian Ministry of Higher Education is offering scholarships for suitable candidates to apply for undergraduate and postgraduate studies in Egyptian universities and institutions for the academic year 2021/2022.

Eligibility

The following general conditions should be met:

  1. Must have a high school certificate or its equivalent for undergraduate candidates.
  2. Must have relevant academic certificates for postgraduate candidates.
  3. Hold a PCR (polymerase chain reaction) certificate 72 hours prior to travel.

List of required documents

  1. A copy of the academic certificates.
  2. A copy of a valid passport.
  3. A recent personal passport size photo.
  4. Certificates and supporting documents must be certified by relevant authorities.
  5. A medical certificate stating that the applicant is free of any infectious disease.

Mode of application and submission  

  1. Complete the online application on the official portal: http://admission.study-in-egypt.gov.eg during the opening period.
  2. Fill your name as stated in the passport, fill in all the required information and attach a copy of your passport and the required documents.
  3. Once the online application is completed, print the application before submitting it electronically.
  4. Submit all required documents during the application opening period to this address: Central Administration for International Students Affairs, 7 Dr. Ibrahim Abu Al-Naga Street, Al Sefarat Neighborhood, Nasr City, Cairo – Egypt.
  5. All queries concerning the scholarship, or the application process should be sent by email to: info@study-in-egypt.gov.eg or call the hotline 19064.
  6. The deadline for online application is September 30th, 2021.

NB: The Government of the United Republic of Tanzania will not provide a loan or grant for candidates who will be offered this scholarship.

Issued by:
Permanent Secretary,
Ministry of education, Science and Technology,
Government City,
Mtumba Area,
Afya Street,
P. O. Box 10,
40479 DODOMA.

RUFAA ACSEE

kwa Matokeo ya Usahihishaji wa Rufaa za Watahiniwa wa Mtihani wa KIDATO CHA SITA (ACSEE) MEI 2021 - AWAMU YA I

BOFYA HAPA 

Jumapili, 1 Agosti 2021

NJIA RAHISI ZA KUSOMA NA KUFAULU MITIHANI YA MWISHO

How to stop falling asleep while studying, how to stay awake while studying, how to stop feeling sleepy, how to stop falling asleep, tips to stop falling asleep, tips to keep awake while studying, tips to stop feeling sleepy
Yawezekana Unasoma sana lakini matokeo yakitoka hutamani rafiki au hata wazazi wako wajue kile ulichopata au unafanya vizuri darasani na mitihani ya kawaida lakini inapofika muda wa kufanya mitihani ya mwisho kama vile ya wilaya,mkoa na taifa unafeli mpaka unahisi unafanyiwa hila au umelogwa!. Kufeli sio jambo zuri kwa mtu kulipata katika kitu chochote hasa ukiwa shuleni,kwa kutambua hilo haijalishi wewe ni mwanafunzi wa shule ya hadhi gani au unarudia mtihani au wewe ni P.C huna budi kujua njia hizi rahisi sana za kukusaidia kufaulu mitihani yako.
Kutoka BORESHA TANZANIA, tumekuwekea mambo mazuri yanayoweza kukusaidia kufaulu mitihani yako ya mwisho kama ifuatavyo;
 

1 . Soma mitihani iliyopita. (past papers)

Njia hii ni rahisi sana itakusaidia sana kujua namna ya kujibu maswali,kujua mitego na mbinu za watunga mitihani ambao mara nyingi hurudia maswali yaleyale kwa namna tofauti, vilevile itakusaidia kujua format au miundo ya mitihani na hii itapelekea wewe kujua majibu ya maswali mengi sana ndani ya muda mfupi sana.
 

2. Jua mada zote za kila somo unalolisoma. (Topics)

Kujua topic za kila somo unalotarajia kujibu mtihani wake kutakusaidia sana kujua mada zipi huwa na maswali mengi,alama nyingi,mada zenye maswali rahisi na magumu.Hii inakupa mwongozo sahihi sana wa kujua wapi pa kuanzia pindi unavyojiaandaa kujibu mtihani.Ni hatari sana kuingia kwenye chumba cha mtihani ukiwa hujui maswali yapi ya kuanza kwenye mtihani husika hata kama unajua vitu vingi vya kujibu.Hivyo kujua topic ni njia rahisi sana kuelekea kufaulu mtihani wako.
 

3. Soma kwa lengo. (target)

Kusoma sio hekali za shamba unazotakiwa kutumia muda mrefu sana ili umalize kuzilima la hasha ! kusoma ni kazi inayohusisha akili na viungo hivyo unatakiwa kuwa na lengo maalumu kila unaposoma sio kusoma ilimradi.Ni heri ulale upumzishe akili kuliko kusoma ukiwa hauelewi kitu husika unachokisoma kina faida gani kwako.Ndio maana wapo baadhi ya wanafunzi wanaotumia muda mrefu kusoma kisha hufeli wakati wapo watu wanaofaulu licha ya kutoingia darasani wala kusoma muda mrefu .Hii ni kwa sababu wengi wa wanafunzi wanaosoma muda mrefu husoma bila ya kujua lengo la kusoma vitu au mada fulani na kuishia kufeli.Hivyo kujua unasoma kitu fulani kwa ajiri gani kutakupa uhakika mkubwa wa kufaulu.
 

4. Tumia muda mwingi kusoma masomo unayoyaelewa vizuri. (uwekejazi)

Usielewe vibaya ! Kutumia muda mwingi kwenye masomo unayoyaelewa vizuri haimanishi uache kusoma masomo mengine,ila hii ina maana kwamba unatakiwa kuelewa zaidi na zaidi na kugeuza masomo yote unayoyaelewa kama uwanja wa nyumbani kiasi kwamba katika mitihani ya masomo hayo unakuwa na uhakika wa kupata zaidi ya 65% mpaka 75% . Mbinu hii ni rahisi sana na muhimu maana ufaulu hutegemea alama za masomo tofauti tofauti na sio somo moja tu.Hivyo jua zaidi kwenye masomo unayoyaelewa yatakulipa kwenye mitihani na kukupa uhakika wa kufaulu.

 

5. Soma notes fupi zenye kubeba mawazo ya msingi. (kupunguzia kichwa mzigo)

Badala ya kusoma maelezo mengi kama msomaji wa risala , Soma notes fupi zilizo andaliwa vizuri zitakusaidia kufaulu mtihani kirahisi.Njia hii itakusaidia kutokuishiwa hamu ya kusoma unapotumia notes fupi,husaidia kuelewa haraka na kwa mujibu wa wataalamu wanadai Notes fupi husaidia sana kumtunzia mwanafunzi kumbumbu nzuri.Hivyo tumia notes fupi, 

 Zingatia

( Hakikisha notes zako fupi zinaendana na kile ambacho mtaala unachohitaji ukisome vilevile Njia hii inaweza kutofanya vizuri sana kwenye baadhi ya masomo mfano hisabati;fizikia na kemia na biologia,hivyo kwa masomo haya notes fupi lazima zipewe uungwaji mkono na mazoezi ya mara).
 

6. Buni kanuni za majibu. (kuwa mbunifu)

Kubuni Kanuni ni ujanja wa aina yake asikudanganye mtu. Elewa kwanza hizi sio kanuni rasmi bali ni kanuni ambazo mtu anabuni kwa namna yake akiwa na lengo zimsaidie kutunza kumbukumbu na zimrahisishie anapojibu maswali.Yawezekana hujaelewa vizuri bado usijali ,,, Mfano mzuri wa kanuni za kubuni ni ule watoto wa shule ya msingi hufundishwa ili kukariri haraka vipimo vya urefu yaani;” Kofia Huuzwa Dukani Mwa Daudi Senti Mia” ikimanisha Kilomita, hektomita, dekamita, Mita,Desimita,Sentimita na Milimita. Hivyo ukitulia kwa kila somo lolote unaweza kubuni kanuni hizi ambazo zitakurahisishia sana kujibu maswali na kukupa uhakika wa kufaulu.

 

7. Fanya tathmini na fahamu muda uliosalia kabla kufanya mtihani. (uandaaji wa silaha)

Hii ni njia rahisi sana inayoweza kukufanya ufaulu mtihani tena ukiwa na uhakika.Tathimini ndio kipimo sahihi kitakacho kufanya ujue upungufu wako uko wapi na nini ufanye kulingana na muda ambao utakuwa umesalia kabla ya kufanya mtihani. Zingatia “tathimini” hii unatakiwa uifanye ukiwa peke yako au na mtu mwenye kukutakia mema kama vile rafiki yako unayesoma naye ,hapo mtagundua wapi panawasumbua na kujua wapi pakupata msaada kabla ya mtihani.Mitihani ya kujiandaa haitoshi kukwambia uko sawa ila inahitaji wewe ufanye tathimini sahihi ujue unachotakiwa kufanya kabla ya mtihani.

 

8. Kutana na wenzako kabla ya siku au masaa machache kabla ya mtihani .(discussion yenye mafanikio)

Hapa elewa kwanza kwenye suala la discussion kuna watu aina mbili darasani au katika kusoma;wapo watu wanopenda sana discussion lakini lazima tuelewe kuwa kuna watu wengine hawapendi kabisa kusikia kitu kama hicho sio kwamba hawapendi ushirikiano na wenzake bali hujisikia huru sana wakiwa wanasoma peke yao.Ikiwa wewe ni miongoni mwa watu wa kundu hili hapa panakuhusu .Raha ya kusoma ni kufaulu hivyo kuna hamu kubwa ya kusoma siku chache kabla ya mtihani .hivyo kama wewe hupendi discussion za kila siku discussion kabla ya kufanya mtihani zitakusaidia sana kujua mbinu za wenzio ukichanganya na zako utapata kitu.chukueni na fanyeni past papers pamoja,utapata pointi nyingi sana na haitakuwa rahisi wewe kuzisahau kama unajiamini kwenye kutunza kumbukumbu nakujibu mtihani kirahisi.
 

9. Elewa mazingira na historia ya mitihani. (kuwa mtabiri)

“ Ni rahisi sana kupata O% kwenye mtihani wa midterm lakini sio rahisi kupata O% kwenye mtihani wa taifa” .Watu hawalielewi hili ,mtihani wa wilaya,mkoa au taifa siku zote unazingatia kupima wanafunzi wa kila aina,wa shule zenye waalimu,wa shule zenye uhaba wa waalimu na hata wale watihaniwa wa kujitegemea.Hivyo maswali hutolewa kwa kuzingatia mtaala wa taifa na sio wa shule wala kituo cha elimu.Kwa kujua hili sio rahisi kufeli ina maana lazima utajua tu maswali ya muhimu ambayo ni lazima yatoke kwenye mtihani ,maana siku zote mtaala wa elimu ni uleule na hata mabadiliko yakitokea serikali hutangaza.Hivyo kwa nini usifaulu mtihani wakati unaelewa mada na maswali yake?!.
 

10.Tulia,kuwa na amani fanya mtihani.( usiwaze kuhusu matokeo,likizo au kumaliza shule)

Tulia!!! Unawaza kuhusu kumaliza mtihani sio?! Tulia ratiba ikiisha utarudi mtaani, hivyo usiruhusu kufikiria mambo mengine badala ya mtihani muda wa mtihani, japo hutokea kwa baadhi ya watu .mfano wale wanaofikwa na matatizo mbalimbali kabla au kipindi cha mtihani sio rahisi kutofikiria matatizo hayo,lakini usijali….Jitahidi kuwa Strong na muombe Mungu. Lakini kama hauna tatizo lolote muda wa mtihani sio muda wa kufikiria kuhusu likizo au nini utafanya baada ya mtihani ,muda wa mtihani ni muda wa kuandaa kile kitakacho onekana baada ya mtihani na si vinginevyo.Ingawa wapo watu wengi sana wanaotumia muda huu vibaya kwa kuwaza nyumbani,na mambo mengine yasiyo sahihi kwa muda huo. Tasisi za Elimu au shule si miaka ya kukufanye ukue bali ni mahali ambapo wazazi,walezi au hata taifa linategemea utoke na ujuzi utakotufaa watu wote hivyo tafadhali usituangushe.
 
ZINGATIA:
Njia hizi ni za uhakika kutokana na mafanikio watu wengi waliotumia njia hizi kufaulu.Kila mtu ni shahidi mazingira ya shule nyingi si rafiki sana kwenye kufaulu kutokana na mapungufu mbalimbali ambayo serikali haiwezi kuyatatua peke yake.Hivyo hakuna wa kumlaumu kwenye matokeo mabovu yanayotokea maana serikali ni mimi,wewe na yule tushirikiane,watu wafaulu nchi iwe na wasomi wenye kuelewa mambo .Lakini tusiishie kufaulu bila ya kuwa wabunifu maana hakuna tutakacho kuwa tunakifanya.soma, faulu, kuwa, mbunifu tupate maendeleo ya kweli.

imeandikwa na
JEROME ERNEST MMASSY
Mwandishi Mwandamizi na Mkurugenzi Mtendaji
Holy Hands Book Project
+255(0) 758 673441

 

Jumanne, 27 Julai 2021

AINA ZA MALEZI NA ATHARI ZAKE

 

Malezi ya watoto ni elimu muhimu yenye ukurasa unaojitengemea. Tumekuwa na kujifunza darasani maada nyingi na muhimu katika maisha yetu, bahati mbaya ni kuwa suala la malezi ya watoto, ambalo kwa kiasi kikubwa wengi wetu laazima tupitie hatua hii limekuwa likiachwa nyuma, na sasa mtazamo binafsi na uhalisia wa mazingira imebaki kuwa njia pekee tegemewa katika malezi na makuzi ya watoto walio wengi.
Namna unavyomlea au kuwalea watoto wako huweza kuathiri moja kwa moja wanavyochukulia mambo na wanavyojichukulia wao, hivyo ni muhimu kutilia maanani njia bora na sahihi inayomjengea motto msingi bora wa maisha yake ya baadae.
Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali juu ya malezi ya watoto, kuna aina kuu nne za malezi, na leo napenda kukushirikisha aina hizi nne na athari zake;
Malezi ya kimabavu.
Tafakari kidogo juu ya sentensi hizi.
• Unaamini watoto wanahitaji uangalizi tu, na si kusikilizwa.
• Unaamini watoto wafuate sheria zako, na si uhalisia uliopo.
• Hutilii maanani hisia za mtoto.

malezi ya kimabavu

Ikiwa katika sentensi hizo apo juu ni sawa kwako, basi aina yako ya malezi ni ya kimabavu. Wazazi katika aina hii ya malezi huamini watoto lazima wafuate sheria na maelekezo yote wanayopewa bila kupuuza wala kukaidi.

Wazazi wenye malezi ya kimabavu, huwaepusha watoto wao na mazingira au vikwazo vinavyowahitaji kutumia akili, badala yake wazazi huunda sheria na miongozo bila kujali mitazamo ya watoto.

Wazazi wenye malezi ya kimabavu, hupenda kusema “mimi nimesema” na inapotokea mtoto anauliza sababu zinazopelekea kupewa maelekezo husika na mzazi wake, mzazi huwa hayuko tayali kufanya mjadala, husisitiza kuheshimiwa tu, na utekelezaji wa alichokielekeza.

Wazazi hutumia adhabu zaidi kuliko kuonya. Hivyo mtoto au watoto hawafundishwi njia za kuepuka makosa, bali wazazi huwafanya watoto wajutie makosa waliyoyafanya.
Athari za malezi ya kimabavu.
Watoto wanaokulia katika malezi ya kimabavu hufuata sheria na maelekezo wakati wote.
Pia watoto hawa hukabiliwa na tatizo la kutokujiamini.

Watoto katika aina hii ya malezi huweza kuwa wakatili na wasiojali hisia za wenzao.

Tafiti zinaonesha kuwa watoto hawa huwa ni waongo wazuri, kwani wamekuwa wakiamini kusema uongo ili kuepuka adhabu.


Malezi ya mamlaka (demokrasia)
Tafakari kidogo juu ya sentensi hizi,
• Unatumia nguvu nyingi kujenga mahusiano mazuri na mtoto au watoto wako.
• Unaelezea sababu zinazopelekea sheria au maelekezo yako kwa watoto wako
• Unatilia maanani hisia za mtoto au watoto wako.

malezi ya mamlaka-demokrasia

Ikiwa katika sentensi hizo apo juu ni sawa kwako, basi aina yako ya malezi ni ya mamlaka. Kama ilivyo kwa wazazi wenye malezi ya kimabavu, wazazi wenye malezi ya mamlaka huweka sheria na miongozo, lakini hutoa nafasi kwa watoto wao kujieleza na kuelezea mitazamo yao.

Wazazi wenye malezi ya mamlaka hutoa nafasi kwa watoto wao kukabiliana na changamoto za maisha, ili kuwajenga.

Pia hutoa maelekezo muhimu kuzuia tabia zisizokuwa nzuri na kusisitiza tabia zenye maadili mema. Hivyo wazazi hupongeza na kusifia tabia nzuri.
Athari za malezi ya mamlaka
Watoto wanaokulia katika malezi ya mamlaka au demokrasia huwa wenye furaha na wenye mafanikio.

Pia watoto hawa huwa na uwezo mzuri wa kufanya maamzi sahihi na kutathmini athari ya maamzi yao.

Tafiti zinaonesha kuwa watoto waliolelewa na wazazi wenye malezi ya mamlaka wanapofikia umri wa watu wazima, huwa wawajibikaji na hujisikia huru kujieleza na kuelezea mawazo yao.


Malezi huru

Tafakari kidogo juu ya sentensi hizi,
• Unaweka sheria na maelekezo, lakini hutilii maanani utekelezwaji wake.
• Huwawajibishi watoto mara kwa mara kwa ukiukaji wa maelekezo na sheria.
• Unaamini mtoto atajifunza vizuri, bila ya kumfuatilia sana.

malezi huru

Ikiwa katika sentensi hizo apo juu ni sawa kwako, basi una malezi huru. Wazazi wenye malezi huru ni wavumilivu, na hawawafuatilii watoto wao sana.

Huingilia na kuonekana pale tu panapojitokeza tatizo kubwa dhidi ya watoto wao.

Wazazi hawa hawawajibishi watoto wao kwa wakati na ikitokea kuwawajibisha hufanya hivyo mara chache zaidi.

Hutoa msamaha zaidi na huamini “mtoto ni mtoto tu” , wanapowawajibisha watoto mara nyingi hutoa msamaha pale mtoto anapoomba msamaha na kuahidi kubadili tabia.

Wazazi hawa huchukua nafasi na jukumu la rafiki zaidi kuliko nafasi na jukumu la mzazi.

Huwashawishi watoto wazungumze matatizo yao, lakini hawafanyi juhudi kubwa kukemea tabia na maamzi yasiyo sahihi ya watoto wao.

Hawakemei tabia nyingi mbovu za watoto wao.

Athari za malezi huru
Watoto wanaokulia katika malezi huru hujituma zaidi kitaaluma, ikiwa wana hulka hiyo.

Watoto hawa hukabiliwa na matatizo mengi ya kinidhamu kwa sababu hawaheshimu utawala wala sheria.

Mara nyingi watoto hawa hawajiamini na muda mwingi huwa ni wenye huzuni.

Watoto hawa huwa na deko lisilo la kawaida, na wazazi hujikuta taratibu wakianza kutumikishwa na watoto wao, bila kujua kuwa tayali wanatumikishwa.

Watoto hawa huwa katika hatari kubwa ya kukubwa na matatizo ya kiafya, hususani meno na tumbo, kwani wazazi hawana muda wa kuwasimamia watoto wao juu ya usafi wa kinywa, chakula na mwili kwa ujumla.


Malezi huria

Tafakari kidogo juu ya sentensi hizi,
• Hufuatilii maendeleo ya watoto wako kitaaluma na kazi zao za shule.
• Mara nyingi hujui wapi mtoto wako yupo na yupo na nani.
• Huna muda wa kukaa na watoto wako.

malezi huria

Ikiwa katika sentensi hizo apo juu ni sawa kwako, basi una malezi huria. Wazazi wenye malezi huria, kimsingi hutarajia watoto wajilee wao wenyewe.

Wazazi hawatumii nguvu nyingi kutafta mahitaji ya watoto wao.

Wakati mwingine wazazi hawa, hawafahamu juu ya maendeleo ya watoto wao.

Mara nyingi wazazi hawa hujikita kutatua shida nyingine tu kama vile kazi, kodi ya nyumba au pango, bili za umeme, maji, ving’amzi, na mahitaji mengine ya nyumbani.

Wazazi hawana ufahamu wa kutosha juu ya wanachofanya watoto wao.

Wazazi huweka sheria na miongozo michache tu.

Hakuna msisitizo wa kutosha katika kuwaelekeza watoto wao, kuwaongoza na kuwajali.

Athari za malezi huria
Watoto waliokulia katika malezi huria, huwa hawana ufaulu mzuri darasani, wala hawajiamini.

Watoto hawa hukumbwa na matatizo mengi ya kinidhamu na huwa hawana furaha.

Hitimisho
Wakati mwingine wazazi hawawezi kuwa katika aina moja ya malezi kikamilifu, wengi huchanganya, lakini ni vizuri zaidi kuwa mzazi mwenye malezi ya mamlaka au demokrasia.

Ukiamua kujitoa na kudhamilia kuwa mzazi bora anayefaa, basi ni vizuri kujenga mahusiano mazuri na mtoto au watoto wako, wakati huo huo ujenge mamlaka yako kwa watoto wako kikamilifu kwa njia ambayo ni rafiki katika makuzi na maendeleo yao, ili baadae watoto wavune matunda ya malezi yako katika maisha yao

 

Ieandaliwa na

tabasamu news