Lebo

Ijumaa, 8 Julai 2022

DHANA YA AKILI NA MAFANIKIO

 SOMO LA KWANZA


*DHANA YA AKILI NA MAFANIKIO*


📙📙📙📚📚📚📚📙📙📙


Sehemu ya TATU 


*Ijue PREFRONTAL CORTEX; sehemu CHANYA ya Akili inayopambana na nguvu HASI (LIMBIC SYSTEM)*





Naendelea kusisitiza kuwa *Ametukuka Mwenyezi-Mungu; mbora wa kuumba*! Katika sehemu ya mbele ya ubongo wa mwanadamu; Kuna sehemu inayoitwa *Prefrontal Cortex*; hii ni sehemu CHANYA inayosimamia mafanikio makubwa ya mwanadamu. Ili kuifahamu vizuri sehemu hii ni vizuri tukajua upande HASI *(LIMBIC SYSTEM)*.


*LIMBIC SYSTEM*



Hii ni sehemu iliyo maeneo ya paji la uso. Huu ni mfumo hasi unaomfanya mwanadamu:

- Awe mvivu

- Apende starehe

- Asipende kujihangaisha

- Akate tamaa mapema

- Aghairishe Mambo muhimu

- Asione umuhimu kusonga mbele n.k.

Mfumo huu unazalisha kemikali iitwayo *Dopermine* (inayozalishwa na Amygdala)  ambayo humfanya mwanadamu Apende kuliwazwa na asipende kabisa kujituma. Umeshawahi kuona Alfajir unataka kuamka lakini kuna kitu kinakubembeleza na kukwambia uendelee kulala!? *Hiyo ndiyo kazi inayofanywa na Limbic system*. Hiki ni kilevi. Kwa bahati mbaya; mfumo huu Mwenyezi-Mungu Amauumba ukiwa kamili kwa 100% tangu Mtoto anapozaliwa!


*PREFRONTAL CORTEX*

Ili kudhibiti nguvu ya Limbic system; Mwenyezi-Mungu Ametuwekea sehemu hii CHANYA ya Prefrontal Cortex. Mfumo huu huwa hauko kamili kimaumbile; huwa inakuwa kadiri mwanadamu anavyojitahidi kupambana na nguvu HASI. Kwa hiyo; jinsi unavyozidi kufanya Mambo ya kimaendeleo na kujituma; mfumo huu unakua na Limbic system hupungua nguvu. Unapoweka malengo makubwa na kuanza kuchukua maamuzi makubwa; unajijengea tabia ya ushundi na mafanikio; hatua kwa hatua.


SWALI:


*Je, umeshawahi kupanga malengo na ukashindwa kutimiza?* Unadhani tatizo gani lilikukwamisha katika kufikia malengo yako!?




mwandishi : Mrisho Said Mbwembe

                          0657942495

mrishombwembwe@gmail.com

@ BoreshaTanzaniafoundation