Lebo

Ijumaa, 1 Julai 2022

DHANA YA AKILI NA MAFANIKIO*

 SOMO LA KWANZA


*DHANA YA AKILI NA MAFANIKIO*




📙📙📙📚📚📚📚📙📙📙

Sehemu ya PILI


*Reticular Activating System (RAS) (Mifumo wa Akili wa kuyaendea malengo).*


Kama tulivyosema kawa Akili ina uwezo na mchango mkubwa Sana katika maendeleo na mafanikio yetu; kitu kinachotakiwa ni sisi kujua uwezo huo na kuufanyia kazi.


Kwenye Ubongo Kuna sehemu iitwayo *Reticular Cortex* ambayo hutengeneza mfumo uitwao *Reticular Activating System (RAS)*. Kazi kuu ya RAS ni kuchuja taarifa na kuratibu namna ya kuweka umakini katika Mambo mbalimbali, kwa kuwa ubongo hufanya kazi kwa mahesabu na kuweka vipaumbele!


Kwa mfano; unapokuwa kwenye mashine ya ATM unataka kufanya muamala; ni rahisi Sana kuikumbuka namba yako ya SIRI ya ATM ingawa ukitoka hapo huwa hauitilii umuhimu kabisaa! Unajua kwanini!? *Ni kwa sababu RAS hutusaidia kuwa makini na Jambo Kama tumeandaa mazingira na tumeamua kulifanya*. Hivyo kila fursa unayoamua kuiendea RAS inakudaidia kuweka mazingira vizuri ili uweze kuwa makini nayo na ufanikiwe.


Leo hii ukiamua kufanya biashara ya kuuza Chakula, Batiki, Nguo za kike, Biriani, Kuku au shughuli yoyote ile; utashangaa kuona unaanza kupata watu au wadau mbalimbali wanaojihusisha na shughuli hizo au wanaohitaji kununua, ingawa kabla ya wazo hilo, ulikuwa huwaoni watu hao. Hivyo, RAS katika ubongo hukusaidia kupata watu na taarifa sahihi kuhusu Jambo unalotaka kulifanya.


Kwa ujumla huwezi kupata watu sahihi au taarifa Muhimu za Jambo fulani hadi uweke malengo na kuamua kulifanya Jambo hilo. Unapoweka lengo na kuanza kulifanyia kazi maana yake unaiambia *Reticular Activating System* iwe tayari kukusaidia kutimiza lengo hilo; kwa kuwa Mwenyezi-Mungu ameitengeneza sehemu hiyo kwa kazi hiyo tu!


Watu wote wanaotimiza malengo yao kwa haraka na kwa mafanikio makubwa huwa wanajenga sifa ya:

- *Kujua wanachokifanya*

- *Kufanya kile wanachokipenda*

- *Kuwa na nia isiyoyetereka* n

- *Kutokata tamaa.*

- *Kuwa karibu na watu sahihi wenye malengo yanayofanana* na

- *Kuendelea kujifunza kila siku*


Jambo kuu hapa ni kuamua kufanya Jambo, shughuli au biashara unayoijua na kuipenda toka moyoni. Utashangaa kuona unapata mafanikio makubwa kwa kuwa Akili hukusaidia kufikia malengo yako.

Usifanye Jambo kwa kufuata mkumbo wala usiache ndoto yako kwa kukatishwa tamaa; jua unachokifanya.


Somo litaendelea kwa uweza wa Mwenyezi-Mungu.


*Naomba utoe ushuhuda kuhusu dhana hii ya RAS Kama umeshawahi kuona uhalisia wake kwenye maisha yako* Kama Kuna swali au maoni weka comment hapa chini.




mwandishi : Mrisho Said Mbwembe

0657942495

mrishombwembwe@gmail.com

@ BoreshaTanzaniafoundation

Maoni 1 :

  1. Najifunza mengi Kila siku kupitia ukurasa huu.

    JibuFuta

share with us