Lebo

Jumamosi, 25 Juni 2022

Ijumaa, 24 Juni 2022

UPDATE KUHUSU AJIRA MPYA ZA WALIMU NA WATUMISHI WA KADA YA AFYA


 Waziri wa Tamisemi  MHE. INNOCENT BASHUNGWA amesema kuwa wiki hii wanatarajia kutangaza ajira mpya za walimu pamoja na watumishi WA KADA ya Afya. 

Waziri ameyasema hayo akiwa katika mkutano na wadau mbalimbali uliofanyika kupitia zoom wakijadiri kuhusu zoezi la uwekaji alama za mipaka tarafa ya Loliondo na maendeleo ya zoezi la uhamaji wa hiari kwa wakazi wa Ngorongoro 

Kuangalia video ya mkutano huo bofya hapo chini 







Jumamosi, 18 Juni 2022

SILSILA YA MASOMO YA AKILI YA MAFANIKIO


MADA 


DHANA YA AKILI

SEHEMU YA KWANZA


Neno AKILI (Mind or Intellect) ni tofauti kimaana na neno UBONGO (Brain); ingawa watu wengi hudhani kuwa maneno haya mawili yana maana moja, la hasha wa kalla!


Kwa kuanzia; neno UBONGO linamaanisha Ogani kubwa iliyohifadhiwa kwenye fuvu la kichwa. Ogani au umbile hili limeundwa na vitu kadhaa ambavyo ni:

- Nyamanyama laini

- Mishipa ya damu (Blood vessels)

- Mishipa ya fahamu (Nerves)

- Chembechembe za damu (Blood cells)

- Tishu (Tissues) mbalimbali na

- Majimaji (Waterly Fluids).

Ubongo umegawanyika katika maeneo makuu matatu ambayo ni:

1. Ubongo wa mbele (Frontal Brain)

2. Ubongo wa kati (Mid brain)

3. Ubongo wa nyuma (Hind brain) ambao unaungana na uti wa mgongo kupitia Medulla Oblongata.



AKILI

Kwa upande wa pili; AKILI ni uwezo uliopo kwenye ubongo unaomuwezesha mwanadamu kuweza kutafakari, kuchambua, kupima, kuchanganua na kutafuta ufumbuzi wa mambo mbalimbali yanayomzunguka.


Ni vigumu kujadili suala lolote la mafanikio na maendeleo bila ya kuhusisha Akili. Labda tuseme kuwa Mafanikio yoyote huanzia kwenye akili ya mtu. ambazo Mwenyezi-Mungu anaziongoza; ndiyo maana wengine husema kuwa, " Man is the product of his own mind.(Mtu ni zao la AKILI yake mwenyewe). Vilevile; James Allen katika kitabu chake cha As the man thinketh anasema wazi kuwa;


"Wewe ni matokeo ya mawazo yanayozunguka akilini mwako kila wakati."; yaani, "You are the product of your dominant thoughts."


Hata katika imani ya dini tunafundishwa kuwa Mwenyezi-Mungu amemfanya mwanadamu kuwa mtawala na kiongozi ( Khalifa ) kwa kumpa uwezo mkubwa wa Akili tofauti na viumba wengine. Kwa hiyo; Mafanikio na maendeleo yote ya mwanadamu na jamii yake kwa ujumla huanzia AKILINI. 


Katika Akili kuna nguvu kuu aina tatu ambazo zinaleta mafanikio makubwa Sana: Kama ukizijua na kuanza kuzifanyia kazi; Je, unataka kuzijua nguvu hizo!!?............


Naam; nguvu hizo ni:


1. Reticular Activating System (Mfumo wa Akili wa kuyaendea malengo)


2. Prefrontal Cortex System (Mfumo wa Akili wa kupambana na hisia hasi)


3. Subconscious mind (Akili nusu razini).


Tutazielezea hizi kwenye somo linalofuata Mwenyezi-Mungu Akipenda.


Somo litaendelea......




mwandishi : Mrisho Said Mbwembe

0657942495

mrishombwembwe@gmail.com

@ BoreshaTanzaniafoundation